Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw. Martin Nkwabi, akifungua mafunzo kwa wastaafu kuhusu huduma za Mfuko wa PSSSF, ambapo wastaafu wa Kanda Ya Ziwa mashariki zaidi ya 100 walipata mafunzo hayo Jijini humo Oktoba 30, 32026
Menaja wa Mfuko wa PSSSF kanda ya Ziwa Mashariki Bw. Rajab Kinande, akizungumza na wastaafu kwenye mafunzo kuhusu huduma za Mfuko wa huo Jijini Mwanza Oktoba 30, 2026.

Baadhi ya wastaafu wa Kanda ya Ziwa Mashariki, waliohudhuria semina ya mafunzo iliyoandaliwa na Mfuko wa PSSSF na kufanyika Jijini Mwanza Oktoba 30, 2026

Mstaafu Bi. Maria Tibaijuika akizungumza kwenye semina hiyo.
Msimamizi kitengo cha Huduma kwa Wateja PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki Bi. Happiness Manyenye, akitoa mada kuhusu umuhimu wa mstaafu kujihakiki.
Mwanza oktoba 30, 2026
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Martin Nkwabi, amesema maisha ya kustaafu ni hatua ya kufunguka kwa fursa mpya ya maisha baada ya kumaliza utumishi na kamwe isichukuliwa kama ndio mwisho wa maisha.
Bw. Nkwabi ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu wanaopokea pensheni katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyofanyika Jijini Mwanza leo. Mafunzo hayo yameandaliwa na PSSSF ili kuwapatia elimu ya namna ya uwekezaji wa kifedha zao baada ya maisha yao nje ya utumishi.
"Kustaafu si jambo baya hata kidogo, bali ni kitu kizuri sana. Huku ndiko kufunguka kwa fursa zingine mpya baada ya kumaliza utumishi katika taifa letu kwa uaminifu. Huu ni wakati wenu sasa wa kupumzika, kufurahi, na kufanya yale mliyokuwa mkitamani kuyafanya mioyoni mwenu kabla hamjaingia kwenye utumishi, niwapongeze sana PSSSF kwa semina hii," alisema Bw. Nkwabi.
Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, Bw. Rajab Kinande, amesema mafunzo hayo yanaakisi kaulimbiu ya PSSSF ya Leo. Kesho Pamoja. Amewasihi watumishi na wastaafu watarajiwa kujiandaa mapema kabla ya kustaafu kwa kuweka taarifa zao kwa usahihi badala ya kusubiri hadi siku ya kustaafu, "Mfuko umeboresha utoaji wa huduma zake, ambapo taarifa za wanachama zimehifadhiwa kwenye mfumo hali inayorahisisha upatikanaji wa huduma ikiwemo Mafao.”
Mstaaafu, Manyama Manyama , ametoa pongezi zake kwa PSSSF kwa kuandaa semina hiyo maalum ya wastaafu, huku akisisitiza umuhimu wa wastaafu kutojiona wanyonge katika jamii kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa kwa Taifa.

No comments:
Post a Comment