MFUMO BORA WA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA JAMII WAANDALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 27, 2026

MFUMO BORA WA UTATUZI WA MIGOGORO KATIKA JAMII WAANDALIWA


Na WMJJWM - Dodoma


Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wadau kutoka sekta mbalimbali wamejadili mfumo bora wa utatuzi wa migogoro katika jamii kwa kutumia njia mbadala.

Majadiliano hayo yanalenga kuweka utaratibu mahususi utakaosaidia kushughulikia migogoro katika jamii kwa njia ya amani, ikiwemo usuluhishi ili kuimarisha mahusiano na mshikamano miongoni mwa wanajamii.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Dkt. Adolar Duwe ameeleza kuwa ili kujenga taifa imara ni muhimu kuwekeza katika familia na jamii kwa kuwa ni msingi wa amani, umoja na maendeleo ya taifa.

Amesisitiza umuhimu wa kuweka mikakati itakayowezesha familia na jamii kutatua changamoto zinazojitokeza kwa njia ya mazungumzo na usuluhishi, hatua itakayosaidia kupunguza migogoro na kuimarisha utulivu katika jamii.

Aidha naye mratibu wa kikao hiko ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wakili Derek Mwajombe ameeleza kuwa kupitia mfumo huo, inatarajiwa kuwepo kwa njia zinazofaa za kupata taarifa pamoja na kushughulikia migogoro nje ya taratibu za kawaida za kimahakama pale inapofaa kwa kuzingatia haki na sheria zilizopo.

Kikao hicho kimewakutanisha wadau wa sekta mbalimbali ikiwemo, OWM - TAMISEMI, Ofisi ya Mwandishi wa Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na wataalam kutoka Wizarani hapa ambao kwa pamoja wameweka maazimio ya namna bora ya kuuboresha mfumo huo.

No comments:

Post a Comment