MHE. RIDHIWANI KIKWETE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA TPSC KAMPASI YA TANGA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 7, 2026

MHE. RIDHIWANI KIKWETE ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA TPSC KAMPASI YA TANGA


Na Veronica Mwafisi-Tanga


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua maendeleo ya ujenzi wa wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tanga na kuupongeza uongozi wa chuo hicho kwa usimamizi mzuri.  

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo, Mhe. Kikwete amesema anafarijika na hatua nzuri aliyoiona ya ujenzi huo. Sisi ndani ya Serikali tunajua umuhimu wa jengo hili, sio pambo bali tunataka kuona majengo haya yanakuwa kitovu cha kutoa elimu katika Mkoa huu wa Tanga. Mhe. Kikwete ameongeza.

Amesema ni matamanio ya Serikali kuona ujenzi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Natamani kuona mwezi Mei 2027 jengo liwe limekamilika na kuanza kutumika ili pia tuweze kuendelea na ujenzi wa majengo mengine ndani ya Kampasi hii. Amesema Mhe. Kikwete.

Amemsihi Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kuendelea kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi ili kukwepa kadhia ya kubadilisha Mkandarasi mwingine pale ambapo watashindwa kufanya kama ilivyofikiwa.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Kikwete kuzungumza, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma katika mkoa huo.

Naye Kaimu Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bi. Prisca Lwangili amemshukuru Waziri Ridhiwani kwa mipango mizuri na namna anavyofanya ufuatiliaji wa mambo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho.

Akiwasilisha taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa ujenzi huo, Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi wa chuo hicho ukikamilika unatarajiwa kuchukua jumla ya wanafunzi 2,000.

Dkt. Mabonesha amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwahimiza utekelezaji wa majukumu yao.

No comments:

Post a Comment