MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOKSI KALAVATI LUSUNGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 7, 2026

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BOKSI KALAVATI LUSUNGO


Na Mwandishi Wetu - Mbozi,Songwe.


​Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa boksi kalavati katika mto Songwe eneo la Lusungo–Senjele, lenye urefu wa mita 16.4, unaotekelezwa kwa thamani ya shilingi milioni 459.348.

​Akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Bw. Michael Mwang’onda, Meneja wa TARURA Wilaya ya Mbozi Mhandisi Jane Mdulla, amesema mradi huo unalenga kutatua changamoto ya mawasiliano na uchukuzi baina ya vijiji vya Senjele na Lusungo pamoja na maeneo mengine ya Mkoa na Wilaya.

​Amesema ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mfuko wa dharura (CERC), baada ya eneo hilo kukumbwa na changamoto ya mafuriko yaliyosababisha na madhara kwenye miundombinu.

​Kwa mujibu wa Mhandisi Mdulla, mradi huo unahusisha ujenzi wa boksi kalavati kubwa la zege pamoja na uwekaji wa alama za barabarani, huku pia kukiwa na ujenzi wa kingo za kuzuia mmomonyoko wa kingo za daraja wenye mita za ujazo 45.

​Uwekaji wa jiwe hilo la msingi unaashiria hatua muhimu katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuimarisha usafiri na usafirishaji, hivyo kuwa chachu kwa shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa maeneo yanayohudumiwa na barabara hiyo mara utakapokamilika.

No comments:

Post a Comment