POLISI SAME WAELIMISHA WANACHUO KUJIEPUSHA NA UHALIFU, DAWA ZA KULEVYA NA UKATILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 28, 2026

POLISI SAME WAELIMISHA WANACHUO KUJIEPUSHA NA UHALIFU, DAWA ZA KULEVYA NA UKATILI








Jeshi la Polisi wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, limeendelea kutoa elimu kuhusu usalama na kuzuia uhalifu kupitia operesheni ya Ongea na Kamanda, Safari hii, operesheni hiyo iliwalenga wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Same, kwa kuwasisitiza kuzingatia maadili, uzalendo na kujiepusha na vitendo vya uhalifu wa aina yoyote.


Akizungumza na wanachuo hao, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Same, SSP Tom Obonyo, amewataka kuzingatia malengo yaliyowaleta chuoni hapo, wakitambua kuwa elimu wanayoipata ni msingi wa kufikia ndoto zao na kulitumikia taifa.

Aidha, SSP Obonyo amewataka wanachuo hao kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya, ikiwemo mirungi, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo, amesema wanafunzi wanapaswa kutambua kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri masomo yao, afya zao na mustakabali wa maisha yao.


Katika hatua nyingine, amewahimiza wanafunzi hao kuwaonea huruma wazazi na walezi wao wanaojitolea kuwekeza katika elimu yao kwa lengo la kuwawezesha kutimiza ndoto zao. Amewataka kutumia muda wao vizuri kwa kuzingatia sababu zilizowaleta Same, kuepuka uzururaji na, badala yake, kujikita katika masomo na shughuli zenye tija kwa maisha yao ya baadaye.


Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kilimanjaro, SSP Asia Matauka, amewasisitiza wanachuo hao kujiepusha na vitendo vya ukatili wa aina yoyote, huku akiwahimiza kuheshimiana na kuzingatia misingi ya usalama katika maisha yao ya kila siku.

SSP Matauka ameongeza kuwa wanachuo hao wanapaswa kuwa makini katika mahusiano yao na kujiepusha na imani za kishirikina zinazoweza kuchochea vitendo vya ukatili, pia amesisitiza umuhimu wa kutatua changamoto kwa njia zinazokubalika kisheria na kutafuta msaada kutoka kwa mamlaka husika wanapokabiliwa na matatizo.


Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Lazaro Mwanyasi, amewataka wanafunzi hao kuheshimu sheria na kanuni za chuo, kusoma kwa bidii na kudumisha uzalendo ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwa wataalamu wenye mchango chanya kwa jamii na taifa.

Wanachuo hao wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa elimu waliyoipata, wakiahidi kuzingatia maadili, nidhamu, utamaduni wa Kitanzania na uzalendo, huku wakijiepusha na mambo mabaya.









<

No comments:

Post a Comment