REA YATUMIA BILIONI 6.8 KUUNGANISHA ZAIDI YA KAYA 100,001 NA GESI ASILIA MIKOA YA LINDI NA PWANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 28, 2026

REA YATUMIA BILIONI 6.8 KUUNGANISHA ZAIDI YA KAYA 100,001 NA GESI ASILIA MIKOA YA LINDI NA PWANI

-Kwa sasa REA imetenga Bilioni 3 kuunganisha Kaya 803 na Taasisi 3 Mkoa wa Pwani

Wakala wa Nishati Vijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Akizungumza katika banda la REA wakati wa maonesho ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati, Mhandisi wa Miradi wa wakala, Mha. Ramadhani Mganga, amesema REA imetumia takribani shilingi bilioni 6.8 kuunganisha kaya 100,001 katika mikoa ya Lindi na Pwani kutumia nishati ya gesi asilia kupikia.

Amesema kati ya kaya hizo, 471 zipo mkoani Lindi, huku nyingine 530 zikiwa katika Kata ya Kisemvule, mkoani Pwani.

Mhandisi Mganga ameongeza kuwa REA imetenga takribani shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kupanua huduma hiyo katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa, hususan Kata ya Kisemvule, ambapo kaya nyingine 803 pamoja na shule tatu zinatarajiwa kuunganishwa na kunufaika na matumizi ya gesi asilia.

Amesisitiza kuwa uwekezaji huo unaonesha mchango wa REA katika kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha wananchi moja kwa moja kupitia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, sambamba na juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo nchini.

Maelezo hayo yametolewa wakati wa hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Mnazi Bay North, Mnazi Bay West, Songosongo na Eyasi Wembere, vilivyopo katika maeneo ya kusini mwa Tanzania.

Hafla hiyo imeshuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

REA imesisitiza kuwa kulingana na upatikanaji wa fedha itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya nishati kufadhili miradi ya kuunganisha kaya na taasisi na huduma ya gesi asilia, ili wananchi wengi zaidi wanufaike na nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira.

No comments:

Post a Comment