
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, akizungumza katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akipokelewa na Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), na Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, (kushoto), wakifurahia burudani ya ngoma za jadi, wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiteta jambo na na Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, (kushoto), katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), na Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, wakiongoza meza kuu katika picha ya pamoja baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, katika mkutano wa mwaka wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Mshauri wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bi. Beatrice Melkiory, akizungumza katika mkutano wa mwaka wa kampuni hiyo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.



Picha za matukio mbalimbali katika mkutano wa mwaka wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, uliofunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha.)
Na. Saidina Msangi, WF, Arusha.
Serikali imeeleza kuwa itaendelea kujenga mfumo wa kodi wa haki, unaotabirika kuwezesha ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini, ili kufikia malengo ya Dira 2050 ya kujenga uchumi wa Dola za Marekani Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050.
Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.
Mhe. Munde alisema kuwa kufikiwa kwa malengo ya Dira 2050 kunategemea juhudi za Serikali na ushirikiano wa karibu na sekta binafsi na kampuni za huduma za kitaalamu kama EY Tanzania.
"Ili kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050, tunahitaji uwekezaji wenye tija kutoka sekta binafsi, taasisi imara, na mfumo wa kodi unaochochea ushindani na ukuaji wa biashara ambapo Serikali imeazimia kuweka mazingira rafiki yatakayomwezesha mlipakodi kutimiza wajibu wake kwa hiari," alisema Mhe. Munde.
Mhe. Munde alifafanua kuwa ili kufikia malengo hayo Serikali itaendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais ya Mapitio ya Mfumo wa Kodi, ikiwa ni pamoja na kuunganisha mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA), pamoja na kutenga asilimia 5 ya rasilimali za Serikali za Mitaa kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya masoko.
Aidha, alisema mifumo ya Tehama na uchanganuzi wa takwimu itaendeelea kuimarishwa ili kupunguza ulazima wa walipakodi kukutana ana kwa ana na maofisa wa kodi, pamoja na kufanya ukaguzi wa pamoja kati ya taasisi za udhibiti.
‘‘Serikali pia itaendelea Kutoa unafuu wa kodi wa mwaka mmoja kwa biashara ndogo mpya zilizoanzishwa, ili kuzipa nafasi ya kukuza mtaji na kutengeneza pamoja na kutekeleza mkakati wa MKUMBI II unaolenga kupunguza mlundikano wa ada na tozo, ambapo Wizara ya Fedha imetenga Sehemu Maalum ya Mapato Yasiyo ya Kodi (Non-Tax Revenue section) kuratibu eneo hilo’’ alifafanua Mhe. Munde.
Mhe. Munde alisisitiza taasisi za kitaalamu na washauri wa kodi kuendelea kutoa ushauri wenye maadili unaolinda uendelevu wa biashara na maslahi ya taifa kwa wakati mmoja, huku ukihimiza elimu ya kodi kuendelea kutolewa kwa jamii.
Mhe. Munde aliwaasa washiriki wa mkutano huo kutumia fursa hiyo ya kimkakati kujadili sera za kodi, fursa za uwekezaji na namna ya kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa ustawi wa uchumi wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Huduma za Kodi wa Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa huduma za ushauri wa kodi, ukaguzi wa mahesabu, na ushauri wa kibiashara ya Ernst &Young-Tanzania, Bw. Donald Nsanyiwa, alisema kuwa Mkutano huo una lengo la kujenga mfumo wa kodi wenye ufanisi, uwazi na unaochochea ukuaji wa uchumi wa Taifa ili kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani bila kuathiri shughuli za sekta binafsi.
Alisema mkutano huo utajikita katika maeneo makuu matatu ikiwemo kuimarisha ushirikiano wa hiari katika ulipaji kodi, kuziandaa biashara kukabiliana na mabadiliko ya kisheria na kisera, pamoja na kujenga uaminifu kati ya walipakodi na Mamlaka ya Mapato (TRA).
‘‘Tutajadili mapendekezo ya mbinu bora za kibiashara ambazo zinaweza kusaidia kuongeza utii wa sheria za kodi na wakati huo huo kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi kwa ujumla. Tutarejea pia baadhi ya hoja na mapendekezo ya kikodi yaliyojadiliwa katika mwaka uliopita, pamoja na hatua zilizochukuliwa na Serikali na namna mabadiliko hayo yanavyoweza kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini’’, alisema Bw. Nsanyiwa.
Aidha, Bw. Nsanyiwa aliongeza kuwa ni muhimu kuwa na majadiliano yenye kujenga ushirikiano kati ya wafanyabiashara, wataalamu wa kodi na Serikali, hasa katika kipindi ambacho kuna mabadiliko mbalimbali ya kisera, kisheria na kiutendaji.
Alisema katika mkutano huo, wataalamu wao watashirikisha uzoefu na maarifa kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika usimamizi na ulipaji wa kodi, pamoja na namna bora ya kuzitatua ili kuhakikisha kwamba mabadiliko yanayoendelea yanaeleweka vizuri na kwamba wafanyabiashara wanakuwa tayari kuyatekeleza.
Bw. Nsanyiwa aliongeza kuwa washiriki wa mkutano huo watapata fursa ya kujadili na kupata uelewa wa kina kuhusu namna ya kuboresha uelewa wa walipakodi kuhusu mifumo mipya ya kidijitali inayotumika katika usimamizi wa kodi kwa kuwa mifumo ya kidigitali imekuwa sehemu muhimu ya usimamizi wa kodi ili waweze kutumia mifumo hiyo kwa usahihi na kwa ufanisi.
Mkutano huo wenye kaulimbiu, (Bolder Thinking, Smarter Tax, Stronger Future), uliwakutanisha washiriki kutoka sekta ya umma na binafsi, wanadiplomasia, wawekezaji pamoja na wataalamu wa kodi.

No comments:
Post a Comment