TFRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA MAONESHO YA PARACHICHI BUSOKELO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 13, 2026

TFRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA MAONESHO YA PARACHICHI BUSOKELO


Na. Mwandishi wetu, BUSOKELO


Afisa Biashara Mwandamizi wa TFRA, Eliakimu Mniko, amesema ushiriki wa mamlaka hiyo katika Maonesho ya Parachichi 2026 unalenga kutoa elimu kwa wakulima wa Busokelo ili kuboresha kilimo chao.

Ameongeza kuwa, eneo hilo limekuwa na mafanikio katika uzalishaji wa parachichi zenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko la dunia, hivyo matumizi sahihi ya mbolea yanaweza kusaidia kuimarisha zaidi uzalishaji huo.

Mkulima Prisca Batayuyu ameipongeza TFRA kwa kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbolea katika Maonesho ya Parachichi 2026, akisema elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa wakulima wa Busokelo kuhusu umuhimu wa kutumia mbolea bora.

Kwa upande wake, Mkulima Kassim Msafiri amesema, elimu aliyopata itamwezesha kuzingatia mahitaji ya udongo katika kilimo cha parachichi, hatua inayotarajiwa kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa mazao yake ili yaweze kushindana katika soko la dunia.

Maonesho ya Parachichi (Avocado Exhibition 2026) yanaendelea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Lwanga, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment