TSKF YATANGAZA UCHAGUZI WA VIONGOZI KUFANYIKA NOVEMBA 2026 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 19, 2026

TSKF YATANGAZA UCHAGUZI WA VIONGOZI KUFANYIKA NOVEMBA 2026


Shirikisho la Mchezo wa Karate Nchini Tanzania (TSKF) limetangaza kuwa uchaguzi wa viongozi wake utafanyika Novemba 21, 2026, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanahabari leo 19 Oktoba, 2026 Jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa TSKF, Jerome Mhagama amesema Fomu za kugombea zitatolewa na kurejeshwa kuanzia Oktoba 22 hadi Novemba 18, 2026, katika ofisi za shirikisho hilo. 


Nafasi zitakazogombewa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu Msaidizi, Mweka Hazina, Mweka Hazina Msaidizi na wajumbe saba.


Ada za fomu ni Tsh 150, 000 kwa Rais na Makamu wa Rais, Tsh 100,000 kwa nafasi nyingine za uongozi na TSh 70,000 kwa wajumbe.

Uchaguzi huo utashirikisha wanachama wanaostahili, huku vyama na klabu vikihitajika kuwasilisha barua na nakala ya cheti cha usajili.

Mhagama ametoa wito kwa wenye sifa na wanaopenda maendeleo ya mchezo wa karate kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa maendeleo ya TSKF.



No comments:

Post a Comment