Baadhi ya Asasi za Kiraia zimeipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kufanya utafiti kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Mkoa wa Arusha.
Pongezi hizo zimetolewa na wawakilishi wa asasi hizo wakati wa majadiliano na THBUB yaliyolenga kukusanya taarifa za l utafiti kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani humo.
Akizungumza Oktoba 21, 2026 wakati wa majadiliano yaliyofanyika katika ukumbi wa Center For Women and Children Development,Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake na Watoto Bi.Hindu Mbwego amesema kuwa anapata faraja kuona THBUB ikitekeleza jukumu lake la kikatiba la kufanya tafiti zinazohusu masuala ya haki za binadamu.
Bi. Hindu amesisitiza kuwa utafiti huo ni muhimu katika kubaini hali halisi ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, changamoto zinazowakabili waathirika pamoja na hatua zinazoweza kuchukuliwa na wadau mbalimbali katika kukabiliana na tatizo hilo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utafiti na Nyaraka wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Paul Sulle amesema kuwa kupitia utafiti huo, THBUB inalenga kupata taarifa zitakazosaidia kuelewa kwa kina changamoto za ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuweka msingi wa mapendekezo yanayoweza kusaidia kuimarisha utekelezaji wa haki za binadamu.
" tuna Imani kubwa kuwa ushirikiano tunaopata kitoka katika taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia na wadau wengine utatupatia matokeo mazuri ya utafiti huu "a mesema Bw. Sulle


No comments:
Post a Comment