Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, akizungumza wakati wa kufungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo, alipowasili katika Ofisi za Hazina Ndogo Morogoro, kwa ajili ya kufungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, (kushoto), akijadiliana jambo na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, katika Ofisi za Mkuu wa Hazina Ndogo - Morogoro kabla ya kufungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Maafisa Utumishi, kutoka Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, wakimsikiliza Mgeni Rasmi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, ambaye ni Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina Bw. Nsubili Joshua (hayupo pichani), yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Afisa Kumbukumbu na Nyaraka kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma, Bw. Felician Rogatian, akitoa elimu kuhusu masuala ya utunzaji wa Kumbukumbu na nyaraka za Serikali kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, wakati wa mafunzo elekezi kwa watumishi hao yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.

Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma nchini, Bw. Georges Ngonyani, akitoa mafunzo kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.


Baadhi ya watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia mafunzo elekezi kwa watumishi hao, yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha, yanayotolewa na Wahadhiri kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo mkoani Morogoro.
(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, WF - Morogoro)
Na. Asia Singano, WF - Morogoro
Watumishi wapya wa Wizara ya Fedha, wametakiwa kuzingatia nidhamu, uadilifu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao, huku wakijenga utamaduni wa kufanya kazi kwa matokeo na kuibua mawazo mapya yatakayoboresha utendaji wa Wizara.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bw. Nsubili Joshua, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi wa Ajira Mpya wa Wizara ya Fedha, yanayofanyika katika Ofisi za Hazina Ndogo Mkoani Morogoro.
Aliwataka watumishi hao kutoa huduma kwa wananchi na wadau kwa wakati na kufuata taratibu zilizowekwa na kulinda mali za taasisi wanazozitumia ili kusaidia Serikali kuyafikia malengo yaliyowekwa kwenye Dira 2050.
‘’Kila mtumishi ni mwakilishi wa Wizara na Serikali huko anakoishi na anakofanyia kazi, hivyo tunapaswa kutoa huduma kwa heshima, usawa, weledi na kwa wakati huku tukizingatia sheria miongozo, na taratibu zinazotuongoza‘’alisema Bw. Joshua.
Amesema mafanikio ya Wizara ya Fedha na Serikali kwa ujumla hayawezi kupatikana kwa juhudi za mtu mmoja au taasisi moja pekee, hivyo watumishi wanapaswa kuzingatia mafunzo hayo ili kupata uelewa utakaoboresha utendaji wao sambamba na kushirikiana, kuheshimiana na kuwasiliana kwa ufanisi na watumishi wengine wa wizara hiyo.
‘’Vilevile mafunzo haya yatawasaidia kufahamu majukumu na mipaka yenu ya kazi, namna ya kushirikiana na watumishi wengine, kutoa huduma bora kwa wadau pamoja na kuzingatia maadili, weledi katika utendaji kazi’’ Alisema Bw. Nsubili Joshua.
Awali, akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo, alisema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo wa kiutendaji na namna bora ya kutekeleza majukumu yao ndani ya Wizara na Serikali kwa ujumla.
“Lengo kubwa la mafunzo haya ni kujenga uwezo wa kiutendaji kwa watumishi hawa ambao ndio wanaanza ajira, ili waweze kutekeleza majukumu ya Wizara ya Fedha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa” alisema Bi. Nombo.
Mafunzo hayo yanayotolewa na Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), - Tawi la Dar-es- Salaam yanahusisha watumishi wa Ajira Mpya 45 wa Wizara ya Fedha, ambao watapata mafunzo kwa siku 10, wakifundishwa mada 18 ikiwemo Muundo wa Serikali na Uendeshaji wa shughuli zake, Utunzaji wa Kumbukumbu, Uendeshaji wa Ofisi, Maadili ya Utumishi wa Umma, Kanuni za Utumishi wa Umma pamoja na masuala mengine ya kiutumishi, kwa lengo la kuwaandaa watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

No comments:
Post a Comment