WAZIRI MASAUNI AAGIZA KUIMARISHWA KWA USAFI NA USIMAMIZI WA TAKA MTO NG’OMBE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 12, 2026

WAZIRI MASAUNI AAGIZA KUIMARISHWA KWA USAFI NA USIMAMIZI WA TAKA MTO NG’OMBE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, ametoa wito kwa Viongozi wakiwemo wa Halmashauri na NEMC kushirikisha wananchi kikamilifu katika kupanga na kusimamia mifumo ya ukusanyaji taka, elimu ya usafi wa mazingira kuimarishwa na Sheria kusimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha mazingira ya Mto Ng’ombe yanakuwa safi na salama.

Waziri Masauni ametoa maagizo hayo Oktoba 11, 2026, wakati wa ziara ya kikazi katika eneo la Mto Ng’ombe, Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kukagua hali ya mazingira na kuimarisha usimamizi wa taka.

Aidha, Mhe. Masauni amesisitiza umuhimu wa kuendeleza zoezi la usafi wa mazingira, ikiwemo kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, ili kujenga utamaduni wa usafi na uwajibikaji miongoni mwa wananchi.

Vilevile, ameelekeza hatua stahiki kuchukuliwa dhidi ya wanaokiuka Sheria na Kanuni za mazingira, wakiwemo wakandarasi wa ukusanyaji taka wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ili kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Masauni amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa juhudi zake za kulinda mazingira, huku akihimiza ushirikiano kati ya baraza hilo, wananchi, mamlaka za serikali za mitaa na wadau wengine katika kuboresha usimamizi wa taka kwa manufaa ya jamii na vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment