Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera ametembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi (U.A.E) ambapo amesaini kitabu cha wageni, na kuzungumza na maafisa Ubalozi.
Ziara ya Dkt. Homera imefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Nishati (ADIPEC) ulioanza Novemba 2 hadi 5, 2026, mkutano huo unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya nishati wakizungumzia masuala mbalimbali yanayoikumba sekta ya nishati ikiwemo usalama na mnyororo wa ugavi wa nishati pamoja na matumizi ya akili Unde (AI) kwenye sekta ya nishati.
Ambapo Tanzania kupitia Wizara ya Nishati imetumia jukwaa hilo la (ADIPEC 2026) kutangaza miradi mbalimbali iliyopo nchini ikiwepo miradi ya mafuta na gesi asilia na miradi ya umeme na nishati jadidifu na kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishati.
Dkt. Homera amepokelewa na Mheshimiwa, Balozi. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed na maafisa Ubalozi.





No comments:
Post a Comment