EAC YAWEKA MIKAKATI YA PAMOJA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO KALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 5, 2026

EAC YAWEKA MIKAKATI YA PAMOJA KUKABILI ATHARI ZA EL NIÑO KALI


Na, Mwandishi Wetu -Nairobi , Kenya


Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinaendelea na mkutano wao jijini Nairobi, Kenya, kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño zinazotarajiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Siku ya pili ya mkutano huo ulioanza Novemba 04, 2026, Maafisa Wakuu wa Usimamizi wa Maafa wa nchi wanachama wa EAC wamejadili mpango wa pamoja wa namna ya kukabiliana na  athari zinazoweza kujitokeza katika Kanda.

Maafisa hao pamoja na mambo mengine wanatathmini uwezo wa nchi wanachama katika kukabiliana na majanga, kubaini mapungufu yaliyopo na kuweka mikakati ya uratibu wa pamoja ili kulinda maisha ya wananchi, huduma muhimu na shughuli za kiuchumi, hususan biashara katika ukanda huo.

Mkutano huo utahitimishwa na Mkutano wa Dharura wa pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Amani na Usalama na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC, utakaofanyika Novemba 06, 2026 kwa ajili ya kuimarisha maandalizi ya kikanda ya kukabiliana na majanga hayo

No comments:

Post a Comment