Na Berema Suleiman Nassor – Zanzibar
Kuwa na bidhaa bora pekee hakutoshi kuhakikisha biashara inakua na kupata soko la uhakika, bali namna bidhaa zinavyofungashwa, kutangazwa na kuwasilishwa kwa wateja ina nafasi kubwa katika kuongeza thamani na ushindani wake sokoni.
Hayo ni miongoni mwa mambo yanayolengwa katika mafunzo ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanavikundi vya watu wenye ulemavu wa Kijaluba iSave yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuboresha biashara zao na kuongeza fursa za kujipatia kipato.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamejikita katika kuwapatia washiriki uelewa wa namna bora ya kufungasha bidhaa mbalimbali wanazozalisha ili ziweze kuvutia wateja, kuhifadhi ubora wake na kukidhi mahitaji ya soko.
Kupitia elimu hiyo, wanavikundi wanapata fursa ya kutambua umuhimu wa kutumia vifungashio vinavyovutia, vyenye ubora na vinavyoendana na aina ya bidhaa wanazozalisha.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa programme wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi wa watu wenye ulemavu na wanajamii kwa ujumla kutoka TAMWA ZNZ Zaina Abdalla Mzee amesema umuhimu wa kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu katika masuala ya biashara ni hatua muhimu katika kukuza uchumi wao na kuwasaidia kujitegemea kupitia shughuli za uzalishaji wanazozifanya.
Alisema uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu wenye ulemavu unapaswa kwenda sambamba na kuwapatia wanavikundi ujuzi unaoweza kuwasaidia kuongeza thamani ya bidhaa zao, kutafuta masoko mapya na kutumia fursa mbalimbali zilizopo ili biashara zao ziweze kukua na kuwa endelevu.
Alisema TAMWA-ZNZ kupitia Programu ya CADiR, imeandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa vikundi vya KIJALUBA iSave yenye lengo la kuwajengea uwezo katika kutafuta na kuendeleza masoko pamoja na matumizi ya vifungashio bora na vinavyovutia wateja.
Alifafanua kuwa Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wanachama kuongeza ushindani wa bidhaa zao na kuimarisha uwezo wa kufanya biashara kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yamewashirikisha wanachama kutoka vikundi 22 vya KIJALUBA iSave vya Unguja, vinavyotoka katika Wilaya za Kati, Kusini na Kaskazini ambapo Vikundi hivyo tayari vimeanza kuzalisha bidhaa mbalimbali baada ya kupata mafunzo ya ujuzi wa uzalishaji, hivyo hatua hii inalenga kuvijengea uwezo wa kutambua fursa za masoko, kuboresha ubora na mwonekano wa bidhaa kupitia vifungashio vinavyofaa, pamoja na kupanua wigo wa wateja ili kuongeza mauzo na kipato.
Kwa upande wake, Afisa Muwezeshaji Muhidini Ramadhan kutoka TAMWA ZNZ amesisitiza umuhimu wa wanavikundi kutumia maarifa wanayoyapata katika mafunzo hayo kuboresha shughuli zao za uzalishaji na biashara, akieleza kuwa elimu ya vitendo ni nyenzo muhimu katika kuwasaidia watu wenye ulemavu kuongeza uwezo wao wa kiuchumi na kujenga mazingira ya kujitegemea.
Nae muwezeshaji wa mafunzo hayo Zainab Jabir Daudi mkufunzi wa masuala ya masoko ambae pia ni mkufunzi wa masuala ya fedha kutoka Wakala wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Zanzibar ZEEA amesema kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa fursa muhimu kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao na kuwafikia wateja wengi zaidi bila kulazimika kutumia gharama kubwa.
Ameeleza kuwa washiriki wanapaswa kujifunza namna ya kupiga picha nzuri za bidhaa, kuziandaa kwa ajili ya matangazo na kutumia majukwaa mbalimbali ya kijamii kuwasiliana na wateja.
Pamoja na hayo alisema ni vyema kwa wanavikundi hao kujenga utamaduni wa kutangaza bidhaa zao mara kwa mara kupitia mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa picha zenye mvuto, maelezo sahihi ya bidhaa na mawasiliano ya uhakika vinaweza kuongeza imani ya wateja na kuchochea mauzo.
Alisema sambamba na matumizi ya teknolojia, mafunzo hayo yameangazia umuhimu wa kushiriki katika maonesho ya biashara kama njia nyingine ya kutangaza bidhaa, kukutana ana kwa ana na wateja na kupata fursa za kuunganishwa na wafanyabiashara wengine.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwasaidia wanavikundi kupanua mtandao wao wa kibiashara na kutafuta masoko mapya kwa bidhaa wanazozalisha.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa elimu waliyoipata imewafungua zaidi kuhusu namna ya kuboresha bidhaa zao, hususan katika matumizi ya vifungashio na utangazaji kupitia mitandao ya kijamii.
Wamesema maarifa hayo yatawasaidia kuondokana na baadhi ya changamoto wanazokutana nazo katika kutafuta masoko na kuwafikia wateja.
Wameongeza kuwa mafunzo hayo ni fursa muhimu kwao, kwani pamoja na kuwapatia ujuzi wa kibiashara, yanawajengea kujiamini na kuwapa hamasa ya kuendeleza shughuli zao za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi na kuchangia maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.
Mafunzo hayo ya siku tatu ni miongoni mwa sehemu ya juhudi za kuimarisha uwezeshaji wa kiuchumi wa vikundi jumuishi vya KIJALUBA iSave, kwa kuhakikisha kuwa wanachama hawabaki katika hatua ya uzalishaji pekee, bali pia wanakuwa na uwezo wa kuuza bidhaa zao na kuendesha shughuli za kiuchumi kwa tija na uendelevu. Mafunzo haya yanaendeshwa na TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na SHIJUWAZA, ZANAB na NAD kupitia Programu ya CADiR.

No comments:
Post a Comment