MAKAMU WA RAIS ATOA ANGALIZO KUHUSU UJENZI WA STENDI YA SH BILIONI 8.4 NAMTUMBO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 11, 2026

MAKAMU WA RAIS ATOA ANGALIZO KUHUSU UJENZI WA STENDI YA SH BILIONI 8.4 NAMTUMBO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 11 Novemba 2026 amekagua mradi wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Namtumbo, akiwa ziarani mkoani Ruvuma.
Mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.4
Stendi hiyo itaboresha huduma za usafiri kwa wananchi, kuongeza mapato ya halmashauri na kufungua fursa za ajira na biashara kwa vijana na wajasiriamali.

Amepongeza jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo katika kusimamia utekelezaji wa mradi huo, lakini akashauri miradi inayotegemea fedha za maendeleo kutoka Serikali itekelezwe kwa awamu ili kuongeza ufanisi na kutoa uhakika wa kukamilika kwa wakati. 

Mradi huo ulioanza kutekelezwa Oktoba 2026 unatarajiwa kukamilika Septemba 2027, huku mkandarasi, kampuni ya AMJ Contractors Ltd, akiwa katika hatua za awali za uchimbaji wa msingi. Kwa mujibu wa Mhandisi wa Mradi, Injinia Allen Mshiru, stendi hiyo itakuwa na maeneo ya kuegesha magari, fremu 197 za maduka, maeneo ya lami, jengo la utawala pamoja na kituo cha polisi.
 
Akizungumza baadaye katika mkutano wa hadhara, Makamu wa Rais amesema Serikali tayari imetoa takribani Sh bilioni moja kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo, ambao unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri, kuongeza mapato ya halmashauri na kufungua fursa za ajira na biashara kwa vijana, wajasiriamali na mama lishe.
 
Katika mkutano huo, Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Profesa Riziki Shemdoe, amesema Serikali pia inaendelea na ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 3.9 pamoja na daraja lenye thamani ya Sh bilioni 1.1 wilayani Namtumbo.
 
Makamu wa Rais ameelekeza barabara hizo ziwekwe taa baada ya kukamilika ili kuimarisha usalama na kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea wakati wa usiku. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kusimamia kwa karibu miradi yote ya maendeleo ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wananchi wanapata huduma bora.

No comments:

Post a Comment