MAZOEZI NA MTINDO BORA WA MAISHA VYATAJWA KUWA SILAHA MUHIMU YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KISUKARI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 14, 2026

MAZOEZI NA MTINDO BORA WA MAISHA VYATAJWA KUWA SILAHA MUHIMU YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KISUKARI

DAR ES SALAAM :Katika kuadhimisha Siku ya Kisukari Duniani inayoadhimishwa Novemba 14 kila mwaka Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania kimeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari.

Elimu hiyo imelenga kuhamasisha jamii kuchukua hatua za mapema kwa kubadili mienendo ya maisha inayoweza kuongeza hatari ya kupata ugonjwa huo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Dk, Rachel Mungu Meneja Mradi wa Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kutoka Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania, amesema kufanya mazoezi mara kwa mara ni moja ya njia muhimu za kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.

Amesisitiza kuwa jamii inapaswa kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa dakika 30 pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali zinazoufanya mwili kuwa katika hali ya uchangamfu.

Dk, Rachel ameeleza kuwa mabadiliko ya mtindo wa maisha ikiwemo kupungua kwa shughuli za kimwili kutokana na maendeleo ya teknolojia na ongezeko la matumizi ya vyombo vya usafiri yamechangia watu wengi kutofanya mazoezi ya kutosha.

Aidha amesema ulaji usiozingatia mlo kamili hususani matumizi ya vyakula vyenye wanga kwa wingi bila kuzingatia mboga za majani matunda na makundi mengine ya vyakula ni miongoni mwa mambo yanayoweza kuongeza hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Kwa upande wake Dk, Monica Appollo Daktrari Bingwa wa Watoto wa kisukari na Magonjwa ya Homoni Kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema watoto asilimia 90 wanagundulika katika mbaya ya kulazwa wakiwa na kisukari hivyo jamii haina uelewa wa kutosha dhidi ya ugonjwa huu.

No comments:

Post a Comment