NGOs ZATAKIWA KUWAJIBIKA MFUKO WA PAMOJA WA RUZUKU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 6, 2026

NGOs ZATAKIWA KUWAJIBIKA MFUKO WA PAMOJA WA RUZUKU


Na WMJJWM- Dar Es Salaam


Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) nchini yametakiwa kuwajibika katika utekelezaji wa uanzishwaji wa Mfuko wa Pamoja wa Ruzuku kwa Mashirika hayo utakaosaidia uendeshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Eliakim Chacha Maswi katika kikao cha Pili cha Kamati ya Kitaifa ya kuratibu mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Pamoja wa Ruzuku kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kilichofanyika Novemba 06, 2026 jijini Dar Es Salaam.

Maswi amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanapaswa kuunganisha nguvu katika kuhakikisha Mfuko huo unasimama na kuimarika zaidi, kwa kujitoa kwao katika usimamizi wake.

"Lazima mjipange na muangalie namna bora ya kuendesha mfuko huu ili ulete tija zaidi na sisi kama Wizara tupo tayari kutoa ushirikiano katika kuweka Mkakati wa pamoja wa kuwa na mfuko utakaosaidia NGOs kutekeleza mipango yenu"
amesema Maswi

Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali NaCoNGO) Jasper Makala amesema mfuko huo utasaidia kuyainua Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hasa madogo ili yajisimamie na kutekeleza miradi mbalimbali ya kusaidia jamii katika kutatua changamoto zilizopo na kuwaletea maendeleo.

Akieleza kuhusu uanzishwaji wa mfuko huo, Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Katibu wa Kamati hiyo Vickness Mayao amesema mfuko huo umeasisiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Septemba mwaka 2021 wakati akizungumza katika Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, ikilenga mfuko huo kusaidia Mashirika hayo kujitegemea katika uendeshaji wa mikakati na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Uanzishwaji wa mfuko wa pamoja wa Ruzuku kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa uendelevu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa mwaka 2022/23-206/27.

No comments:

Post a Comment