TIMU YA KUVUTA KAMBA WANAWAKE YA TUME YA MADINI (MC) YAHITIMISHA SHIMMUTA 2026 KWA KISHINDO, YATWAA KOMBE NA MEDALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 21, 2026

TIMU YA KUVUTA KAMBA WANAWAKE YA TUME YA MADINI (MC) YAHITIMISHA SHIMMUTA 2026 KWA KISHINDO, YATWAA KOMBE NA MEDALI


Timu ya kuvuta kamba wanawake kutoka Tume ya Madini (MC) imehitimisha kwa mafanikio ushiriki wake katika Mashindano ya 56 ya SHIMMUTA 2026 baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mchezo huo na kujinyakulia kombe pamoja na medali.

Katika mashindano hayo yaliyohitimishwa Novemba 21, 2026, katika Viwanja vya Jamhuri, mkoani Morogoro, timu hiyo imeonesha kiwango cha juu cha ushindani, mshikamano, nidhamu na ari ya ushindi kwa kupambana vikali dhidi ya timu mbalimbali zilizoshiriki.

Katika mchezo wa kuvuta kamba, Tume ya Madini ilishika nafasi ya pili, huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na timu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi, kujituma, nidhamu na ushirikiano miongoni mwa wachezaji, pamoja na maandalizi yaliyoiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Ushiriki wa Tume ya Madini katika SHIMMUTA 2026 ni sehemu ya kuimarisha mshikamano, afya, mahusiano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa taasisi za umma kupitia michezo.

Kwa upande mwingine, Mashindano ya 57 ya SHIMMUTA yanatarajiwa kufanyika Julai 2027, mkoani Arusha, ambapo timu ya Tume ya Madini inatarajiwa kurejea kwa ari mpya ili kuendeleza mafanikio na kuiwakilisha taasisi hiyo kwa ushindani zaidi.

No comments:

Post a Comment