WAZIRI MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA TANZANIA MKUTANO COP 31 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 10, 2026

WAZIRI MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA TANZANIA MKUTANO COP 31

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya maandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (COP 31) kilichofanyika Nocemba 9, 2026 Antalya, Uturuki. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Richard Muyungi
Wataalamu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia kikao cha kupitia taarifa ya maandalizi ya ushiriki i wa Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (COP 31) kilichofanyika Antalya, Uturuki kilichofanyika Novemba 9, 2026, Antalya, Uturuki.
Wataalamu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia kikao cha kupitia taarifa ya maandalizi ya ushiriki i wa Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (COP 31) kilichofanyika Antalya, Uturuki kilichofanyika Novemba 9, 2026, Antalya, Uturuki.


Na Mwandishi Wetu 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ameongoza kikao cha viongozi na wataalamu kupitia taarifa ya maandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi (COP 31).

Kikao hicho kimefanyika Novemba 9, 2026, Antalya Uturuki ikiwa ni siku kwanza ya ufunguzi wa Mkutano huo uliotanguliwa na mkutano wa Watalaamu kujadili vipaumbele vya majadiliano ya mkutano huo mwaka 2026.

Waziri Masauni amehimiza umuhimu wa ujumbe wa Tanzania kuweka msisitizo katika kuimarisha diplomasia ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi na vipaumbele muhimu vitakavyoongoza majadiliano ya mkutano huo.

Amebainisha vipaumbele hivyo ni pamoja na upatikanaji wa fedha, kujenga uwezo kwa wataalamu na umuhimu wa kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Ni muhimu kusisitiza kwa wadau, wabia wa maendeleo na mashirika ya kimataifa umuhimu wa kuiwezesha Tanzania kupata fedha na kujenga uwezo kwa wataalamu wetu ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi” amesema Waziri Masauni.

Aidha amesema pia ni muhimu kwa ujumbe wa Tanzania kusisitiza umuhimu wa matumizi rasilimali na maliasili za asili zilizopo nchini ili ziweze kutumika vyema katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amesema ujumbe wa Tanzania umejipanga vyema katika kuhakikisha wanapasa sauti katika majadiliano hayo na kusisitiza utekelezaji wa makubaliano yaliyowekwa.

“Tumepanga kukutana na wadau na mashirika ya kimataifa ili kuweza kukumbusha ahadi mbalimbali zilizotolewa ikiwemo upatikanaji wa fedha na kusisitiza umuhimu wa kujenga uwezo kwa wataalamu” amesema Dkt. Muyungi.

Ushiriki wa Tanzania katika COP31 utatoa fursa ya kuitangaza nchi kimataifa kwa kuonesha hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kauli mbiu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo inasema “Hatua jumuishi za Tanzania za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya Dira 2050: Kujenga Taifa Imara, la Kijani na lenye ustawi”

No comments:

Post a Comment