Baraza la Mawaziri la Raisi Magufuli...Unaambiwa Wabunge Sasa Hivi Matumbo Joto - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 24, 2015

Baraza la Mawaziri la Raisi Magufuli...Unaambiwa Wabunge Sasa Hivi Matumbo Joto


WAKATI Rais John Pombe Magufuli akitegemewa kutangaza Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa, matumbo ya wabunge yamepata moto wakijiuliza kama watawezana na kasi yake endapo watateuliwa kuwemo.

Magufuli, ambaye Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimuita Tingatinga, ameweka wazi katika hotuba yake kwa Bunge kuwa hatamvumilia mtu mzembe na mvivu na kwamba watakaobainika kujihusisha na rushwa au ufisadi, watashughulikiwa.
Ingawa wabunge karibu wote walikuwa wakimshangilia kwa nguvu wakati wa hotuba yake hiyo, inadaiwa hamu ya kupata ulaji wa uwaziri inawafanya baadhi yao kuingiwa na woga, kwani ufanyaji kazi wa mazoea ndiyo unaowatesa.

“Nakuambia hapa wabunge, hasa wale wenye ndoto za kuteuliwa uwaziri wana wasiwasi kama wataweza kweli kwenda na kasi ya huyu jamaa, maana anaonekana kuwa siriaz sana na kazi. Hili liko wazi maana wengi walizoea kuona nafasi za juu kiuongozi wanazitumia kwa masilahi yao,” kilisema chanzo chetu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Inadaiwa wengi wa wanaotegemea kupata uwaziri wana hofu kwa sababu wanaamini mzigo watakaopewa utakuwa mkubwa kuliko tabia na hulka zao.

Rais Magufuli ameahidi kuteua Baraza dogo la Mawaziri litakalokuwa limesheheni wachapakazi na katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi, alisema kazi hiyo ataifanya kwa dhati.
Hata hivyo, mbali na jina la Tingatinga hivi sasa mtaani amepewa jina jipya la Mtumbua majipu licha ya kuwa kitendo hicho huleta maumivu.

No comments:

Post a Comment