Lowassa Awatembelea Wahanga Waliookolewa Mgodini Baada ya Kufukiwa Kifusi Kwa Siku 41 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 24, 2015

Lowassa Awatembelea Wahanga Waliookolewa Mgodini Baada ya Kufukiwa Kifusi Kwa Siku 41


Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa Jana alitoa shilingi milioni mbili kwa wahanga waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

Akikabidhi fedha hizo kwa wahanga hao, Lowassa alisema ametoa fedha hizo kama msaada ili ziwasaidie kwa matibabu kwa muda wote watakapokuwa hospitalini hapo, ambapo kila mmoja amepatiwa shilingi laki tano.

Mmoja wa wahanga hao, Joseph Burule alisema kitendo cha Lowassa kuwatembelea hospitalini hapo kimewapa faraja kubwa, kwani tangu waokolewe na kuanza kupatiwa matibabu hakuna kiongozi mkubwa aliyefika kuwajulia hali pamoja na kuwapa pole.

Burule alisema kitendo hicho kinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi pindi linapotokea jambo la kusikitisha kama hilo, na kusema kuwa fedha hizo zitawasaidia kujikimu hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA Salome Makamba aliwaambia wananchi waliojitoza kumsabahi Lowassa kuwa, Lowassa amekuja kuwapa pole wahanga hao na hakuja kwa masuala ya kisiasa.

Novemba 15, 2015 wahanga 5 kati ya 6 waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya nyangalata wilayani kahama waliokolewa wakiwa hai baada ya kukaa ndani ya mashimo kwa siku 41, ambapo juzi mmoja kati yao alifariki dunia.

Ni hivi karibuni baada ya kuokolewa mmoja wa wahanga hao alikaririwa akimuulizia Lowassa kama alishinda urais wa  Tanzania kwenye uchaguzi na baada ya kuambiwa hakushinda alikosa raha.

No comments:

Post a Comment