Baadhi ya Mikoa ya Pemba na Unguja wameanza kushusha bendera za CHADEMA, hawakubaliani na uteuzi wa viti maalum.
Wanadai Zanzibar ilitakiwa ipate nafasi tano za Viti maalum.
Makamu mwenyekiti wa BAWACHA Zanzibar Hamida Abdallah Aweshi amesema wamechoka na ukandamizaji na maamuzi yaliyofikiwa na Chama hicho kutokana na mgawanyo wa hafasi za Viti maalum vya Ubunge, amesema makao makuu ya CHADEMA wamekataa kusikilizwa kilio chao. Amesema wamekosa sehemu ya kupeleka kilio chao.
No comments:
Post a Comment