Katika soka baadhi ya namba za jezi
uwanjani huwa zinaheshimika kubwa uwanjani na wakati mwingine unaweza
kukuta klabu wameiweka jezi pembeni kwa sababu hawaoni nani ataitendea
haki na kulinda heshima yake. Jezi namba 7 ni miongoni mwa jezi zenye
heshima kubwa katika klabu ya Manchester United na moja kati ya watu walioipatia heshima jezi hiyo ni David Beckham na Cristiano Ronaldo.
Memphis Depay aliyesajiliwa msimu huu na klabu ya Manchester United akitokea klabu ya PSV Endhoven ya Uholanzi kwa dau la pound milioni 25 anavaa jezi hiyo kwa sasa. Depay ambaye kwa wiki za karibuni amekuwa akikaa benchi na Jesse Lingard
kuchukua nafasi yake, amekuwa akitajwa kuwa na presha kubwa kutokana na
wengi kutaka kuona anaifanyia makubwa jezi namba 7 kama walivyofanya Cristiano Ronaldo na David Beckham.
Baada ya maneno mengi kuongelewa juu ya jezi namba 7 David Beckham amempa ushauri Memphis Depay kuwa hatakiwi kuwa na presha au kuogopa kuvaa jezi hiyo licha ya kuwa inatajwa kuwa na mafanikio makubwa Man United lakini ni heshima kwake kuvaa jezi namba saba.
“Sioni
kama jezi namba 7 inatisha au kuogopesha chochote mimi nafikiria ni
heshima kuivaa, unapopewa jezi namba 7 haina maana ya kwamba hadi uwe
umeshinda au huyo mchezaji awe amepata mafanikio sana, lakini mwisho wa
siku ni jezi maalum kuivaa ila sifikirii kama inakuwa na presha kuivaa
binafsi ni jezi inayonihamasisha uwanjani” >>> Beckham
No comments:
Post a Comment