Baada ya Adele kuonyesha nia ya kutaka kufanya remix ya Hotline Bling, kumekuwa na minongono juu ya mtazamo wa Drake kwenye ishu hiyo, watu wengi ikiwa mashabiki wamekuwa wakitaka kujua nini kinaendelea kichwani mwa Drake juu ya ombi la msanii huyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa etalk, Drizzy Drake ameonyesha pia nia kubwa sana ya kufanya remix hiyo na Adele muda wowote atakapokuwa tayari… “Nitafanya kitu chochote na Adele, hata akitaka niende kwake kumsaidia kufua nitaenda, nipo tayari hata sasa hivi“, alisema rapper huyo.
Alipoulizwa kama atakuwa tayari pia kumfundisha Adele style za uchezaji wa ngoma hiyo, Drake aliuambia mtandao wa etalk
kuwa angependa kufanya hiyo lakini hatojua pa kuanzia kwani style zote
alizokuwa anazicheza zilikuwa kama freestyle na sio kwamba alifanya
mazoezi popote…
>>> “Sikupanga
kucheza vile, zile style zilikuja natural, na nia ilikuwa kuwafanya
watu wapate muamko wa kujiamini pale wanapoisikia ngoma yangu. Na kuona
dunia nzima imeipokea kwa namna walivyoipokea inanifurahisha sana.” <<< Drake.
No comments:
Post a Comment