Kwa sababu tayari Rais wa John Pombe Magufuli ametangaza
 kwamba sherehe za Uhuru siku ya December 09 2015 hazitokuwepo, ninayo 
taarifa nyingine kuhusu maamuzi mengine ya pesa ambazo zilitengwa kwa 
shughuli hiyo.
Taarifa kutoka Ikulu imetolewa kwamba 
fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kutumika kugharamia sherehe za siku
 ya Uhuru ambazo zingefanyika December 09 2015, zitumike kufanya upanuzi
 wa barabara ya Mwenge hadi Morocco iliyopo Dar es salaam yenye urefu wa
 kilometa 4.3 kwa kuongeza njia za barabara za lami.
Taarifa hiyo ya Ikulu imesema tayari 
fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa 
barabara TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
Hii hapa taarifa yote ya Ikulu.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kubadilisha matumizi ya pesa, kama unakumbuka siku alipolihutubia Bunge November 20 2015
 aliagiza zaidi ya Milioni 200 zipelekwe kununulia vitanda vya wagonjwa 
hospitali ya Muhimbili badala ya kutumika kwenye sherehe za Wabunge 
Dodoma… kama ulipitwa na hiyo, video yake hii hapa.

No comments:
Post a Comment