Ukiachia kufuta safari zisizo za lazima kwa watumishi wa umma tayari amewaondoa baadhi ya watendaji ambao wamekutwa na makosa mbalimbali yaliyoliletea Taifa hasara.
Leo makampuni mbalimbali ya umma na taasisi za Kiserikali zimekutaka katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es salaam kuzungumzia mikakati yao kufuati agizo la rais la kuondoa matumizi yasiyo ya lazima.
Lawrance Mafuru ambaye ni msajili wa hazina amezungumza na viongozi mbalimbali wa makampuni na kusema “Kila mtu ambaye yupo kwenye eneo la kutoa huduma kwa jamii anatakiwa kuhakikisha anaondoa kero kwenye huduma zake, tujifunze kutoka katika makampuni binafsi”.
“Tuna benki za kutosha kama Serikali, tumenunua mabehewa lakini tumefuata utaratibu? inashangaza kuona ni mabovu,,wamekagua lakini bado wameletewa mabehewa mabovu, wale wote mliopewa nafasi kusimamia makampuni makubwa kama haya”.Lawrance Mafuru
List ya mikakati tunayotakiwa kufanya kwenye taasis zenu…“Makatibu wakuu waliitwa na Rais na kupewa maelekezo mbalimbali, tunapaswa kufanya majukumu yetu kwa ufasaha, kama unatakiwa kutengeneza umeme utatakiwa kufanya kwa wakati..Serikali na taasis zake ifanye kazi pamoja, kila mmoja aheshimu mamlaka na nafasi ya mwingine”.
“Taasisi ambazo zina kazi ya kutoa huduma kwa jamii mfano maji, umeme zifanywe kwa sera zilizopo, hawatakiwi kujazana hazina wakidai hawana pesa, wanatakiwa kutafuta namna ya kuendeleza miradi yao, tutaipa Serikali changamoto ya kuongeza mitaji,,sio kila kitu lazima tufanye na wageni, tuitumie Serikali kwa moyo”.
Baadhi ya kampuni hazifanyi ukaguzi wa mahesabu …“Ukiwauliza kwa nini wanasema hawana fedha, hakutakuwa na msamaha kama kampuni inashindwa kufanya odit kwa miaka zaidi ya mwaka mmoja, tutamtaka CAG aongeze ukaguzi, na zile kampuni zinazodai hazina pesa zijitokeze na kujieleza”..
No comments:
Post a Comment