Anthony Martial ameipa Manchester United wasiwasi mkubwa baada ya kuondoka Uwanjani Wembley Jana Usiku akitembelea Magongo.
Martial, mwenye Miaka 19, Jana aliichezea France ilipofungwa 2-0 na
England katika Mechi ya Kirafiki na kuumia Mguu wake wa Kushoto na
kutolewa nje katika Dakika ya 67.
Wakati akiondoka Wembley baada ya Mechi hiyo Mguu wa Kushoto wa
Straika huyo ulifungwa Bendeji nzito na alikuwa akitembea kwa msaada wa
Magongo.
Hali hii itampa wasiwasi mkubwa Meneja wa Man United Louis van Gaal
ambae anamtegemea sana Chipukizi huyo aliefunga Bao 5 tangu ahamie hapo
Septemba 1 akitokea AS Monaco ya France.
Kocha wa France, Didier Deschamps, ameeleza Martial aliumia juu ya Mguu karibu na Vidole.
Huyu ni Mchezaji wa Pili wa Man United kuumia katika Wiki hii ya
Mechi za Kimataifa baada ya Kiungo Michael Carrick kuumia Ijumaa
iliyopita akiichezea England ilipofungwa 2-0 na Spain huko Alicante.
Jumamosi Man United inacheza Ugenini na Watford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Baada ya Mechi za Novemba 8, Ligi kusimama kupisha Mechi za Kimataifa
Jumamosi Novemba 21
1545 Watford v Man United
1800 Chelsea v Norwich
1800 Everton v Aston Villa
1800 Newcastle v Leicester
1800 Southampton v Stoke
1800 Swansea v Bournemouth
1800 West Brom v Arsenal
2030 Man City v Liverpool
Jumapili Novemba 22
1900 Tottenham v West Ham
Jumatatu Novemba 23
2300 Crystal Palace v Sunderland
No comments:
Post a Comment