Gazeti
kubwa nchini Uingereza, Daily Mail limepamba picha ya mshambuliaji wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta akishangilia bao lake alilofunga
katika ushindi wa 2-0 dhidi ya USM Alger mjini Lubumbashi jana kwenye
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Samatta alifunga la kwanza la pili
akafunga Rogger Assale na kufanya ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali
kushinda pia 2-1 mjini Algiers wiki iliyopita. Samatta alifunga pia
Algiers na ndiye ameibuka mfungaji bora wa michuano ya mwaka huu kwa
mabao yake saba. |
No comments:
Post a Comment