Mualiko
huu unaitaka timu ya taifa ya Mpira wa miguu wa Ufukweni, Zanzibar Sand
Heroes kushiriki kwenye mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe
16-20 mwezi wa Disemba, 2015 kwenye fukwe za Buntwani, kata ya Kilifi,
mji wa Malindi nchini Kenya.
ZFA
kimepokea mualiko huo kwa moyo mmoja kikiamini kwamba ni mwendelezo
mzuri wa kukuza ushirikiano na wenzao wa Kenya kwenye michezo lakini pia
kuona kuwa Zanzibar Sand Heroes ni moja kati ya timu zitakazopeleka
changamoto kwenye mashindano yao.
Chama hicho kinaamini hatua hiyo imekuja kufuatia ziara iliyofanywa mwezi Disemba mwaka jana na timu ya taifa ya Beach Soccer kutoka Uganda ‘Uganda Sand Cranes’ hapa nchini kuwa yenye mafanikio makubwa.
![]() |
Kikosi cha Zanzibar Sand Heroes |
Chama hicho kinaamini hatua hiyo imekuja kufuatia ziara iliyofanywa mwezi Disemba mwaka jana na timu ya taifa ya Beach Soccer kutoka Uganda ‘Uganda Sand Cranes’ hapa nchini kuwa yenye mafanikio makubwa.
Lakini
mbali na ziara hiyo, pia kuwepo kwa ligi ya Beach Soccer ambayo kwa
asilimia kubwa sana kupitia vyombo vya habari kuitangaza vyema kulitoa
msukumo mkubwa wa kutambuliwa na kufuatiliwa na nchi jirani.
Timu
inatakiwa ilipe gharama za usajili (Registration fee) ambazo ni
Shilingi Elfu tano za Kenya (Ksh. 5000) au Dola 50 za Kimarekani. Mbali
na gharama hiyo ya usajili timu inatakiwa ijilipie yenyewe gharama za
usafiri wa kwenda na kurudi nchini humo.
Kwa
upande wa kamati ya mashindano ambayo inaoongozwa na Madam Melda
Munyazi itatoa huduma za Chakula, Malazi, Usafiri na huduma nyengine
zinazohusiana na mashindano hayo.
Kwa
sasa chama hicho cha soka visiwani Zanzibar kinajipanga kuthibitisha
ushiriki wao baada ya kukutana na kamati ya Beach Soccer ambayo
imekubali kuupokea mualiko huo.
ZFA
inaamini endapo Wazanzibar watashirikiana kwa pamoja timu za Zanzibar
Sand Heroes na ile ya Zanzibar Heroes zitaleta ubingwa ndani ya nchi
ufuatia mashindano yanayowakabili mbele yao.
Kwa
mara ya mwisho kikosi cha Zanzibar Sand Heroes kilishuka dimbani
Disemba 7 mwaka jana kwenye fukwe za Bamboo maeneno ya Bububu nje kidogo
ya mji wa Zanzibar kucheza na wageni wao kutoka Uganda 'Uganda Sand
Cranes' kwenye pambano la kirafiki la kimataifa ambapo Zanzibar
walikubali kichapo cha bao 5-4.
Kwa
upande mwengine kikosi cha awali cha Zanzibar Heroes kilichotangazwa na
kocha msaidizi Malale Hamsini Keya kinatarajiwa kuanza mazoezi rasmi
hapo kesho majira ya saa 12:30 asubuhi uwanja wa Amaan chini ya kocha
huyo akisaidiwa na kocha wa Makipa Saleh Machupa huku kocha mkuu wa
kikosi hicho Hemed Suleiman 'Moroko' akiwa kwenye kambai ya Taifa Stars
nchini afrika ya Kusini.
No comments:
Post a Comment