Nina Wasiwasi na Naibu Spika Kama Atalihimili Bunge Hili - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 20, 2015

Nina Wasiwasi na Naibu Spika Kama Atalihimili Bunge Hili

Sina wasiwasi na elimu yake wala uwezo wake wa kujieleza, ila nina wasiwasi na hekima yake na busara zake kama zinaweza kustahimili mikiki mikiki ya bunge kama alivyoonyesha Anne Makinda.

Nafikiri wote tunaujua uwezo wa Prof. Muhongo kielimu lakini alifeli somo la hekima.

Najua bunge lina sheria zake kanuni zake miiko yake na desturi zake, lakini ni mara ngapi tumeona sheria zikikiukwa na wabunge wenyewe.

Kama tukisema yeye atakuwa "Iron Lady" kuwa kila mbunge akikosea anamhukumu kulingana na kanuni atafukuza wangapi, naje kama atafukuza karibu nusu ya wabunge ataonekana ni Naibu Spika mzuri au kiti kimemshinda.

Tuchukue mfano wa refa wa mpira wa mguu anayewatoa wachezaji kwa red kadi kila wanapofanya rafu, hivi timu ikibaki na nusu ya wachezaji huyo refa atakuwa bora?

Najaribu tu kumwangalia huyu Naibu Spika asije siku moja akatoa machozi kwa kuzomewa au kuulizwa maswali ya kuudhi akakiaibisha kiti.

Namuomba sana Spika Job Ndugai ajaribu kumsaidia msaidizi wake.

Tujadili kwa mstakabali wa nchi yetu.

By QuinineJamii Forums

No comments:

Post a Comment