Na Sixmund Begashe, Dodoma
Taasisi za uhifadhi Wizara ya Maliasili na Utalii, zimetakiwa kutekeleza Sheria na Kanuni za uhifadhi ili kuwawezesha wananchi kunufaika na urithi wa Maliasili uliopo nchini.
Dkt. Kijaji, ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma, kwenye kikao chake na wataalam wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Maliasili na Utalii na Idara ya Wanyamapori na Idara ya Utalii, kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja wa Sheria na kanuni za uhifadhi wa Wanyamapori.
Pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri ya uhifadhi, amesisitiza kuwa, ni dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mhifadhi namba moja, kuhakikisha watanzania wananufaika na uhifadhi wa urithi wa maliasili zilizopo, hivyo ni vyema wakati wa kufanya mapitio ya Sheria au kanuni zinazosimamia uhifadhi kuzingatia hilo.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Utalii, Bw. Nkoba Mabula, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amemuhahidi Waziri Kijaji, kuhakikisha maelekezo aliyotoa yanatekelezwa kwa uhifadhi na Utalii endelevu nchini.






No comments:
Post a Comment