
Na. Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo-Dar es salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ni muhimu kwa Taasisi ya UONGOZI kuendelea kuwaandalia program za Uongozi Watumishi wa Umma wenye mwelekeo wa Uongozi leadership potential ili kuwa na Viongozi watakaokuwa na uzalendo na weledi katika taifa.
Waziri Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 23 Januari, 2026 jijini Dar es salaam alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mhe. Kikwete amesema, uamuzi wa kushirikisha wafanyakazi wa Taasisi za Umma, binafsi na za kiraia katika program hizo unatoa fursa kwa washiriki hao kubadilishana uzoefu na kuboresha utendaji.
Amesema ni wakati sahihi wa kuweka mikakati ya ujenzi wa Kituo cha Uongozi (Leadership Center) ambacho zaidi kitawajengaViongozi katika Utumishi wa Umma.
Akihitimisha hotuba yake Mhe. Kikwete ameipongeza Menejimenti na Watumishi wote wa Taasisi ya Uongozi kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ofisi hiyo ambapo ameomba ushirikiano Ili kwa pamoja waweze kumsaidia Rais katika kutekeleza majukumu ya Utumishi na Utawala Bora.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Bw. Kadari Singo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi yake, aliwashukuru Viongozi hao kwa kuwatembelea na kuhimiza uwajibikaji na kuahidi kuyafanya kazi maelekezo watakayopewa.





No comments:
Post a Comment