Wananchi wa Mabatini Wapongeza Miradi ya Maendeleo katika Siku 100 za Rais Samia - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 24, 2026

Wananchi wa Mabatini Wapongeza Miradi ya Maendeleo katika Siku 100 za Rais Samia


WAKAZI wa kata ya Mabatini mkoani Mwanza wamepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika eneo lao, wakisema imeleta maboresho makubwa ya kiuchumi na kijamii ndani ya siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kata ya Mabatini, kuna mradi wa ujenzi wa daraja la Mabatini

Akizungumza jana wakati wa mahojiano malumu mkazi wa Mabatini, Nyakasama Makore alisema ujenzi wa daraja la Mabatini na uwekaji wa taa za barabarani umesaidia kupunguza athari za mafuriko na kurahisisha shughuli za biashara. Alisema kwa sasa wakazi wa Mabatini wanafanya kazi mpaka usiku.

Kwa upande wake, msimamizi wa mradi wa Mabatini kutoka Nyanza road works Kulwa Chigugu, alisema kuwa uboreshaji wa miundombinu umeongeza usalama, kurahisisha usafiri na kusaidia wafanyabiashara pamoja na vijana kupata ajira na kipato. Alisema kupitia mradi huo wameweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya 60.

Naye mkazi wa Mabatini, Mariam Samweli, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapelekea mradi wa taa za barabarani, akisema zimepunguza vitendo vya uhalifu na kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kiuchumi hadi nyakati za usiku.

Amesema wanaendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za kijamii ikiwemo kampeni za usafi wa mazingira, huku wakieleza matumaini makubwa ya kuendelea kunufaika na miradi mingine ya maendeleo.

Vile vile katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja na barabara katika kata ya Mkuyuni mradi huo unaendelea vizuri huku mkandarasi akiendelea na kazi za umaliziaji.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mradi,Sefrosa Lyatuu alisema mkandarasi wa mradi huo Jasco Company kwa sasa anajenga mitaro na tayari ameshaweka taa za barabarani katika baadhi ya maeneo ya mradi.

Alisema kabla ya daraja hilo eneo la Mkuyuni lilikuwa linasumbuliwa na mafuriko haswa katika kipindi cha Masika.

Alisema daraja hilo limefikia hatua ya asilimia 99 na linaelekea kukamilika.

“Tunaishukuru Serikali kwa kufadhili na kuendelea kusimamia mradi huu. Barabara na daraja vitasaidia kurahisisha usafiri na kukuza biashara kwa wananchi,”

Kwa upande wake, mmoja ya wanufaika wa mradi huo Charles Ndelema, alimshukuru Rais Samia kwa kuwaletea wananchi mradi huo muhimu.

“Mradi huu utarahisisha usafiri kwa wananchi. Pia umetusaidia sisi wafanyakazi kupata kipato na kuimarisha maisha yetu,” alisema Ndelema.

Amepongeza juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu, wakieleza matumaini kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment