Michezo
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inayojiandaa kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Algeria, imeendelea na mazoezi ya kujiweka sawa kuelekea mchezo huo utakaopigwa November 14 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na November 17 kurudiana Algeria.
Kabla ya kucheza mchezo huo Taifa Stars itacheza mchezo mmoja wa kirafiki Jumapili ya November 8 dhidi ya timu ya chuo kikuu cha Pretoria Tucks FC jijini Johannesuburg Afrika Kusini, kocha wa Taifa Stars Charles Mkwasa ameomba kucheza mchezo huo ili kupata nafasi ya kuangalia kikosi chake kabla ya mchezo na Algeria.
Taifa Stars wapo Johannesuburg Afrika Kusini kwa kambi ya siku 10 kabla ya kurejea Dar Es Salaam kucheza mechi dhidi ya Algeria, Stars inafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa ajili ya kujiweka sawa na inatumia viwanja vya St. Peters College na kituo cha michezo cha Edenvale.
No comments:
Post a Comment