Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay tayari ameingia ndani ya Bunge Dodoma Tanzania… Proj. Jay
amesema amefurahi kwa kuaminiwa na wananchi wa Mikumi Morogoro kwa
kuchaguliwa kuwa Mbunge, amefurahi na anaamini kuanzia sasa ataendelea
kushughulikia majukumu yake kama Mbunge.
Joseph Haule+Joseph Mbilinyi
ndani ya Bunge… YES, ni majina makubwa kwenye Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yaliyochimbukia muziki wa Rap Bongo… wao wamesema
ni wawakilishi wa wale waliowachagua na kazi yao ni kuhakikisha
wanatumikia wananchi kwa kutekeleza ahadi.
Shavu jingine limewakuta Yamoto Band kufanya collabo na mkongwe Dully Sykes… Dully amesema tayari video ya mdundo wao imekamilika na kwa sasa wanatarajia kuachia video siku ya Ijumaa wiki hii.
Kama hujui mama yake Dully Sykes ni shabiki wa muziki wa Hip Hop, Dully amesema kwa sasa mama yake anasikiliza sana wimbo wa Joh Makini Feat. AKA– Don’t Bother.
Msami Feat. Tekno? Good news ikufikie kwamba Msami Baby mkali wa kuimba na kudance ambaye aliibukia THT tayari ana collabo na Tekno kutoka Nigeria ambaye amekamata headlines sasahivi na mdundo wa ‘Duro‘.
Msami amesema mipango inayofatia sasahivi ni kujiandaa kuachia ngoma hiyo watu waisikie pamoja na video kama mambo yakienda sawa.
No comments:
Post a Comment