AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma
kuwa kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa
Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza.
Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa
imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa
mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla
ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili
iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa
mikopo.
Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote
mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti
ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa
ajili ya taratibu za usajili.
Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye
sifa kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830,
wanapata mikopo.
Aidha, Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati
mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
No comments:
Post a Comment