Hivi majuzi muhubiri maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua aliwasili nchini kwa kile kilichoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Mwananchi kwamba muhubiri huyo amekuja nchini kushuhudia kupishwa kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli.
Alipowasili uwanja wa ndege hapa Tanzania alipokelewa na baadhi ya viongozi walioongozwa na Dr. John Pombe Magufuli na akaenda moja kwa moja kumsalimia Rais Kikwete Ikulu magogoni Dar es Salaam.
Baada ya kutoka Ikulu muhubiri huyo alielekea nyumbani kwa aliyekuwa mgombea urais wa UKAWA na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa eneo ambalo ameonekana kuwepo kwa Muda mrefu akizungumza na Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA.
MASWALI
1. Je, ujio wa Muhubiri huyo ilikuwa ni msafara binafsi Kinyume na ilivyoripotiwa na vyombo vya habari?
2. Vyombo vyetu vya habari havikupewa taarifa sahihi kuhusu sababu za ujio wa kiongozi huyo?
3. Kama ni msafara binafsi kwanini apokelewe na rais mteule na kutembelea Ikulu?
4. Je ni viongozi wa UKAWA wamemzuwia kuhudhuria sherehe hizo za kupishwa Rais kutokana na wao kugomea kusaini matokeo?
5. Je, bado yupo nchini? Maana kama tulijulishwa kuhusu ujio wake si vibaya tukajuzwa kuhusu kuondoka kwake.
Nawasilisha:
No comments:
Post a Comment