Wabunge wa UKAWA wameamua kubadili gia angani ili kuhakikisha rais Magufuli hahutubii Bunge.
Wamesema si haki wala haileti picha nzuri kwa mtu ambaye hajashinda
Urais kihalali kwenda kuhutubia bunge tukufu. Wamesema watahakikisha
hahutubii.
Wabunge hao wamesema Safari hii hatatoka nje ya Ukumbi wa Bunge, bali
watahimizana kuhudhuria kwa Wingi Bungeni, watakachokifanya wao ni
kupiga kelele na kuimba nyimbo za UKAWA hadi Rais ashindwe kuongea.
Wanajivunia Wingi wao bungeni, wanajivunia umoja wao wa UKAWA.
Wanasema bunge hili la 11 ni tofauti na Mabunge yalopita kwani UKAWA
wamekuja na mbinu mpya ya kuwadhibiti CCM na kuhakikisha hakuna kitu
kinapitishwa kiholela na UKAWA wamepanga kutumia mbinu moja kati ya
nyingi siku ya Rais kuhutubia na kufungua Bunge.
Hawezi akahutubia bunge ambalo halina Wabunge wa Zanzibar.
CHANZO JAMII FORAM
No comments:
Post a Comment