Mhe. Sekiboko ametoa rai hiyo Machi 17, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati hiyo kwenye mradi wa ujenzi katika Kampasi ya Mloganzila.
Amesema kazi iliyofanyika ni kubwa na kwamba nchi inakwenda kuzalisha wataalamu wabobezi katika maeneo mbalimbali ya tiba hivyo ni vizuri kampasi hiyo ikafahamika kwa elimu inayokwenda kuitoa lakini kwa kazi iliyofanyika kukiboresha na kuongeza fursa za mafunzo na tafiti.
Akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa majengo katika Kampasi ya Mloganzila unaogharibu zaidi ya Shilingi Bilioni 77 amesema
unakwenda vizuri ukiwa asilimia 80 na kwamba Kamati imeridhishwa na kasi na ubora wa kazi.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaleta manufaa makubwa, ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi, pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Amesisitiza kuwa upanuzi wa Chuo cha MUHAS unakwenda kupunguza uhaba wa madaktari na wataalamu afya nchini.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Afya (MUHAS), Profesa Emmanuel Balandya, amesema eneo la Kampasi hiyo lina jumla ya ekari 3,800 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa kimkakati na mingine.
Profesa Balandya ameongeza kuwa kukamilika kwa miundombinu hiyo kutaimarisha shughuli za ufundishaji, utafiti sambamba na utoaji wa huduma za kibingwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo magonjwa ya moyo na mishipa ya damu na mishipa ya fahamu
Naye Msimamizi Msaidizi wa Mradi wa HEET katika Chuo cha Muhas, Profesa Nathanael Siliri, amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa Kampasi ya Mloganzila ni kuifanya kuwa mji mkuu wa kitaaluma wa tiba, wenye vituo vya umahiri vitakavyotoa huduma za hali ya juu na kufanya tafiti zitakazosaidia maendeleo ya sekta ya afya nchini na ukanda wa Afrika Mashariki.









No comments:
Post a Comment