Gazeti hili ambalo pia lilikuwepo kwenye viwanja hivyo vilivyosheheni mastaa wa fani mbalimbali, liliwaona wawili hao ambao awali walikuwa marafiki wakubwa, wakijivinjari kwa tahadhari ili wasikutane, licha ya nyakati tofauti kuzungumza na mastaa wengine.
Wema ambaye katika kampeni za CCM alikuwa pamoja na Makamu wa Rais, aliyekuwa mgombea mwenza Samia Hassan Suluhu, wakiwa na kundi lao maarufu la Mama Ongea na Mwanao, muda mwingi alionekana akiwa na wenzake aliokuwa nao ‘timu moja’ kwenye kampeni.
Aunt Ezekiel ambaye wakati wa kampeni hizo alikuwa kundi lililopewa jina la Nimestuka, naye alijichanganya na waalikwa wengine lakini jicho lake likiwa makini kuhakikisha hakutani hata sehemu moja na muigizaji huyo wa Filamu ya Madam.
Katika sherehe hiyo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa kitaifa wa serikali iliyopita, akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mkewe, mama Salma Kikwete na waziri mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga na mkewe.
Mastaa wengine waliojumuika katika hafla hiyo iliyochagizwa na muziki kutoka kwa Yamoto Band ni pamoja na mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi, Ally Choki, muigizaji mkongwe, Bi Mwenda, mlezi wa wasanii Mama Loraa na Emmanuel Mbasha.
GPL
No comments:
Post a Comment