Msanii ambaye yuko kwenye orodha ya wasanii wakubwa wa Tanzania
waliowahi kufanya vizuri sana miaka ya nyuma, Lucas Mkenda maarufu kama
Mr Nice amethibitisha kwamba ni kweli huwa anakunywa pombe na kulala
bar.
Akiongea na Planet Bongo ya EATV amesema watu wanaosema kuwa amefulia ni waongo tu na kuhusu tetesi kuwa ni mlevi wa kutupwa na analala Bar, Mr Nice ameweka wazi kuwa yeye anakunywa na kulala Bar sababu ana pesa za kuweza kufanya hivyo na anakunywa mpaka pale anapotosheka.
Mkali huyo wa Takeu amewataka wasanii wa kibongo wanaojisifia kwa mali na mbwembwe wawe wakweli na kuonyesha mali zao za ukweli kama ambavyo yeye ameonyesha nyumba ambayo anadai ni yake na kukanusha ile taarifa ya kuwa kwa sasa hana hata sehemu ya kuishi.
Source: Eatv.tv

No comments:
Post a Comment