Usiku wa December 2 ilikuwa ni zamu ya kuchezwa kwa mechi za Copa del Rey nchini Hispania, michezo nane ilichezwa usiku wa December 2 ila mchezo uliyochezwa mapema zaidi ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Villanovense uliyopigwa katika dimba la Nou Camp.
Kwa sasa FC Barcelona
unaweza kuita ndio timu inayoongoza kwa safu bora ya ushambuliaji
kutokana na ushindi wa mechi zao za hivi karibuni kuibuka na ushindi wa
idadi kubwa ya magoli, matokeo ya mechi zao nne zilizopita zinaonesha
kuwa walimfunga Real Madrid 4-0 LALIGA, wakamfunga AS Roma 6-1 UEFA, wakamfunga Real Sociedad 4-0, lakini usiku wa December 2 wameifunga Villanovense goli 6-1 katika mchezo wa Copa del Rey.
Kwa takwimu hizo FC Barcelona wanakuwa wamefunga jumla ya goli 20 ndani ya mechi nne, ambapo ni sawa na wastani wa goli 5 kwa kila mechi, magoli ya FC Barcelona yamefungwa na Daniel Alves dakika ya 4, Sandro Ramirez dakika ya 21, 31, 69 na Munir El Haddadi dakika ya 51 na 76 wakati goli pekee la Villanovense lilifungwa na Juanfran dakika ya 29.
No comments:
Post a Comment