
Na Mwandishi wetu.
Jamii imetakiwa kuzingatia misingi ya dini ili kuwa na jamii yenye maadili, upendo na mshikamano wa kitaifa na hofu ya Mungu.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba alipokuwa akifunga mashindani ya kuhifadhi Qur'an Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.
Dkt. Mwigulu amesema kuwa, malezi thabiti ya vijana katika kumcha Mungu ni muhimu hapa nchini kwa kuwa yatasaidia kuandaa viongozi wenye hofu ya Mungu na kuipenda nchi yako kwa uzalendo mkubwa.
Ameipongeza ofisini ya Mbunge wa Kondoa kwa kuandaa mashindano huku akiahidi kuwa, ofisi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zote za namna hiyo.

Naye Mbunge wa Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, amesema kuwa, lengo la mashindano hayo, ni kukijenga kizazi chenye kuzingatia misingi ya dini kwa maslahi mapana ya Taifa na maendeleo yake.
Katika mashindano hayo ya sita, Kijana Yasir Omari kutoka Kijiji cha Busi kaebuka kidedea kwa kuhifadhi kichwani Judhuu 30 na kujishindia shilingi Milioni 1, nafasi yapili ikishinda na Almas Rashid kutoka Masange, aliye jishindia Shilingi laki 8 na Osama Ally, Kondoa Mjini akiibuka mshindi wa tatu na kijioatis shilingi laki 6.





No comments:
Post a Comment