Diamond Platnumz |
MWANAMUZIKI wa Afro Pop, Diamond Platinum anatamani kuachia ngoma
nyingine lakini amekiri kupata kikwazo kutokana na matokeo ya Wimbo wa
Nana aliouachia mara ya mwisho.
Diamond au Chibu amefunguka kuwa kwenye ‘library’ yake ana nyimbo nyingi
kali ambazo zipo tayari kuachiwa muda wowote lakini kutokana na Nana
kuendelea kufanya vizuri mpaka sasa tangu alipoiachia anaona bora
aendelee kusubiri, asifululize kuingiza kazi nyingi sokoni kwa wakati
mmoja.
“Unajua vitu vipya vipo, lakini nimecheki
upepo naona kama bado kwanza kwa sasa maana Nana bado inafanya vizuri,
nataka kuipa muda kwanza kabla sijaachia ngoma mpya japokuwa nia yangu
kubwa ni kuachia wimbo kabla ya mwaka haujabadilika, kwa hiyo bado
nacheki,” alisema Diamond.
Nana ambao amemshirikisha Flavour wa Nigeria, umewika vizuri Afrika na
kufanikiwa kumpa baadhi ya tuzo ikiwemo ya Wimbo Bora wa Kucheza wa
Mwaka (AFRIMMA), Mtumbuizaji Bora (MAMA), Msanii Bora wa Mwaka (MTV
EMA), Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (AFRIMA) na nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment