Klabu ya soka ya wanawake ya BAOBAB QUEENS mkoani Dodoma,itakayoshiriki ligi ya Taifa ya wanawake,inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya wanawake kutoka kata ya Nzuguni,NZUGUNI QUEENS katika uwanja wa Shule ya Sekondari Nzuguni.
Kwa muujibu wa msemaji wa timu hiyo,JOSEPHIN KAPONYA,Mchezo huo utapigwa leo majira ya saa kumi jioni 4:00,ikiwa ni maandalizi ya kuelekea ligi yaTaifa ya wanawake
Timu 12 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Taifa ya Wanawake inayotarajiwa kuanza Novemba mosi, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Soka la Wanawake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoridhia tarehe hiyo.
Kutakuwa na jopo la makocha watakaofanya uteuzi wa wachezaji nyota watakaoitwa kwenye timu za taifa ambaye atagharamiwa na TFF.
Hata hivyo, Vyama vya soka katika mikoa shiriki, vimeombwa kuvisaidia vilabu vyao katika bajeti zao kwa vile tathamini inaonyesha kuwa fedha zinazotoka hazitoshi. Vyama hivyo vya mikoa pia visaidie maandalizi ya michezo kama vile kuandaa uwanja na kadhalika ukioandoa waamuzi ambao watagharamiwa na TFF.
Katika ligi hiyo,hakutakuwa na zawadi ya fedha zaidi ya kombe la medali kwa timu shiriki, labda kama atatokea mdhamini mwingine,pia hakutakuwa na zawadi kwa mchezaji bora, mfungaji bora, kipa bora, ingawa kutakuwa na jopo la kuwachagua. Mchezaji bora atachaguliwa kwenye hatua za mwisho wa mashindano, mfungaji bora atachaguliwa kuanzia hatua ya kwanza ya mashindano.
No comments:
Post a Comment