NGAO YA JAMII :VEYULA VS MJI MPWAMPWA HAPATOSHI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 21, 2016

NGAO YA JAMII :VEYULA VS MJI MPWAMPWA HAPATOSHI DODOMA



Okuly Julius & Dayi Matalu,Dodoma

Michuano ya ligi ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kumtafuta bingwa mpya wa mkoa 2016/2017, inatarajia kuanza kutimua vumbi katika Wilaya nne zilizopangiwa kuwaka moto,Oktoba 26 mwaka huu.

Kabla ya ufunguzi huo  kutapigwa pambano la ngao ya jamii tarehe 23/10/2016 kwenye dimba la Jamhuri kwa kuwakutanisha mabingwa wa kombe la DOREFA, Timu ya MJI MPWAMPWA kutoka wila yani Mpwapwa dhidi ya Mabingwa wa ligi ya mkoa 2015/2016, timu ya VEYULA FC kutoka Dodoma mjini .

Kiingilio katika mtanange huo kimetajwa kuwa ni sh.1000 za kitanzania kwa muujibu wa katibu mkuu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Dodoma ,HAMIS ISSA KISOI,huku wadau na mashabiki wakiombwa kujitokeza kwa wingi kushudia pambano hilo ambalo ni kiashiriaa cha ufunguzi wa ligi hiyo.

Baada ya ngao hiyo,mechi za ufunguzi zitakazokuwa katika makundi manne zitachezwa ambapo Kundi A GWASSA FC VS SUPER STARS (DODOMA MJINI),Kundi B, KM CHEPA VS AJAX FC (KONDOA), Kundi C,MUUNGANO FC VS SABASABA FC (CHEMBA-MRIJO),na Kundi D,KONGWA UNITED VS VIPAJI FC (KONGWA),Michezo yote itafunguliwa tarehe 26/10/2016.

Sambamba na mechi hizo za ufunguzi, michuano hiyo itaendelea katika makundi hayo manne yenye timu saba kila kundi huku kundi D likiwa na timu 8 na kukamilisha timu 29 shiriki katika ligi hiyo.
  
Licha ya makundi hayo kuwa na timu nyingi,kila kundi litatoa timu mbili kwa ajili ya kupata timu 8 bora huku washindwa wawili bora (Best  looser) zitachukuliwa kukamilisha timu kumi zitakazocheza fainali kwa mfumo wa ligi.

Fainali hizo zinatarajiwa kuchezwa katika Wilaya ya MPWAPWA kwa ajili ya kumpata bingwa wa mkoa atakaewakilisha mkoa wa DODOMA katika ligi ya mabingwa ya mkioa Tanzania bara mwakani.

No comments:

Post a Comment