Kwamba
Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 13:00hrs Katika Eneo La Buswelu Kata Ya
Buswelu Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Wakiwa Katika
Misako Na Doria Walifanikiwa Kuwakamata Watu Sita Wakiwa Na Silaha Mbili
Zilizotengenezwa Kienyeji Pamoja Na Risasi Ishirini Na Tatu, Ambazo
Walikuwa Wakizitumia Katika Matukio Ya Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji
Hapa Jijini Mwanza Na Mikoa Mingine.
Aidha
Tukio Hilo Limefanikiwa Baada Ya Kupokea Taarifa Kutoka Kwa Raia Wema
Kuhusu Uwepo Wa Wahalifu Hao, Ndipo Askari Walifanikiwa Kumkamata Kwanza
Jeremiah Maligia @ Mkumbo Miaka 25, Mnyiramba, Fundi Seremala Mkazi Wa
Malega – Singida Ambaye Alipohojiwa Alikiri Kuhusika Na Kutaja Wenzake
Waliokuwa Wakishirikiana, Na Kuwa Silaha Wamezificha Kwa Mganga Wa
Kienyeji Aitwaye Leornad Litta @ Makai Anayeishi Mtaa Wa Kagida –
Buswelu.
Askari
Walikwenda Mahali Hapo Na Kufanikiwa Kumkamata Mganga Huyo Wa Kienyeji
Bwana Leornad Litta Miaka 39, Akiwa Na Silaha Hizo Mbili
Zilizotengenezwa Kienyeji Hapo Nyumbani Kwake Na Risasi Ishirini Na
Mbili Zinazotumiwa Na Bunduki Ya Aina Ya Short Gun Na Risasi Moja Ya
Rifle Aina Ya Mark Iv.
Aidha
Katika Kuhojiwa Zaidi Na Askari Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Waliwataja
Washirika Wao Wanne Ambao Walikuwa Wakishirikiana Katika Kufanya Uhalifu
Ambapo Askari Walifanikiwa Kuwakamata, Ambao Ni 1. Kamgisha Jovini
Kamhambwa Miaka 40, Mlinzi Na Mkazi Wa Iloganzala, 2. Juma Yusuph @ Jimi
Miaka 35, Mkazi Wa Bwani Kinondoni, 3. Samweli Peter Miaka 36, Mkazi Wa
Busweli Na 4. Shabani Hussein Miaka 26, Fundi Viatu Na Mkazi Wa Nyasaka
Msumbiji.
Watuhumiwa
Wote Walipofanyiwa Mahojiano Walikiri Kwamba Silaha Hizo Walizitumia
Katika Unyang’anyi Wa Mali Na Uporaji Katika Maeneo Ya Jiji Na Mkoa Wa
Mwanza, Aidha Jeshi La Polisi Kwa Sasa Linaendelea Na Uchunguzi
Kuhusiana Na Tukio Hilo Na Matukio Waliyokuwa Wameyafanya, Pindi
Uchunguzi Ukikamilika Watuhumiwa Wote Watafikishwa Mahakamani.
Kamanda
Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa
Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuendelea Na Tabia
Ya Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Lao La Polisi, Ili Tuweze Kudhibiti
Uhalifu Katika Mkoa Wetu., Lakini Pia Anatoa Angalizo Kwa Wananchi Haswa
Vijana Akiwataka Kuacha
Tabia Ya Kujihusisha Na Uhalifu Bali Wajikite Katika Kufanya Shughuli Halali Za Maendeleo, Kwani Jeshi La Polisi Lipo Vizuri
Kuhakikisha Ulinzi Na Usalama Upo Kwa Raia Wote Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza.
Katika Tukio La Pili
Mnamo
Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 14:00hrs Mchana Katika Eneo La Ilemela
Wilaya Ya Ilemela Jiji Na Mkoa Wa Mwanza, Askari Walifanikiwa Kuwakamata
Watu Wawili Ambao Ni 1. Rahim Feka Miaka 28, Mkazi Wa Ilala – Dar Es
Salaam, 2. Ally Kawalale Miaka 32, Mkazi Wa Jetrumo – Arport Dar Es
Salaam, Wakiwa Wanataka Kuuza Gari Lenye Namba T.778 Azv Aina Ya Toyota
Land Cruiser Lililokuwa Wameliiba Huko Ilala Jijini Dar Es Salaam.
Aidha
Watuhumiwa Hao Walikamatwa Baada Ya Kupokelewa Taarifa Ya Kuibiwa Kwa
Gari Hilo Huko Dar Es Salaam Na Kwamba Kuna Uwezekano Kuwepo Eneo La
Kanda Ya Ziwa, Ndipo Ulifanyika Upelelzi Kuhusiana Na Taarifa Hiyo, Na
Kufanikiwa Kuwakamata Watuhumiwa Tajwa Hapo Juu Wakiwa Na Gari Hilo.
Watuhumiwa
Wote Wapo Chini Ya Ulinzi Wa Jeshi La Polisi Wakiendelea Na Mahojiano ,
Huku Taratibu Za Kuwasafirisha Kwenda Dar Es Salaam Wakiwa Chini Ya
Ulinzi Wa Askari Polisi Zikiwa Bado Zinaendelea.
Kamanda
Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa
Rai Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kuacha Tabia Ya
Kununua Vitu Vya Wizi, Bali Pindi Wanapoona Biashara Za Wizi Zinataka
Kufanyika Au Zinafanyika Watoe Taarifa Polisi Ili Watuhumiwa Waweze
Kukamatwa Na Kufikishwa Mahakamani.
Katika Tukio La Tatu
Kwamba
Tarehe 18.10.2016 Majira Ya Saa 23:00hrs Katika Kitongoji Cha Ibungiro
Kijiji Cha Sagani Kata Ya Kandawe Wilaya Ya Magu Mkoa Wa Mwanza, Mtu
Mmoja Msichana Aliyejulikana Kwa Jina La Dema Charles @ Bulayi Miaka 20,
Mkazi Wa Kandawe, Ameuawa Kwa Kukatwa Na Vitu Vyenye Ncha Kali Sehemu
Za Kichwani Na Kiunoni
Akiwa Amelalala Na Watu Wasiojulikana, Huku Wenzake Wa Wili Wakijeruhiwa Sehemu Mbalimbali Za Miili Yao.
Majeruhi
Waliojeruhiwa Katika Tukio Hilo Ni 1.mariam Lucas @ Kapele Miaka 26,
Mkazi Wa Kijiji Cha Sagani Aliyejeruhiwa Shingoni Na Kwenye Kiganja
Cha Mkono Wa Kulia, 2. Kapelele Makubi @ Salulo Miaka 90, Ambaye Ni Baba
Mwenye Nyumba/ Mji, Aliyejeruhiwa Mgongoni, Kichwani Na Kiunoni.
Inadaiwa
Kuwa Wauaji Hao Walifika Katika Nyumba Hiyo Majira Tajwa Hapo Juu Na
Kuwakuta Wenye Mji Wakiwa Wamelala, Ndipo Waliingia Ndani Na Kufanya
Mauaji Hayo, Hadi Sasa Hakuna Mtu Yeyote Aliyekamatwa Kuhusiana Na Tukio
Hilo.
Aidha
Uchunguzi Wa Awali Umebainisha Kuwa Mauji Hayo Yametokana Na Kulipiza
Kisasi, Jeshi La Polisi Kwa Sasa Lipo Katika Upelezi Pamoja Na Uchunguzi
Kuhusiana Na Tukio Hilo, Majeruhi Wapo Katika Hospitali Ya Wilaya Ya
Magu Wakiendelea Kupatiwa Matibabu Na Hali Zao Zinaendelea Vizuri.
Kamanda
Wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Naibu Kamishina Wa Polisi Ahmed Msangi Anatoa
Wito Kwa Wakazi Wa Jiji Na Mkoa Wa Mwanza Akiwataka Kutoa Ushirikiano
Kwa Jeshi La Polisi Ili Watuhumiwa Wa Mauaji Hayo Wawezwe Kukamatwa Na
Kufikishwa Katika Vyombo Vya Sheria.
Imetolewa Na:
Dcp: Ahmed Msangi
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
No comments:
Post a Comment