EL DERBI MADRILEÑO: RONALDO HETITRIKI, REAL YAIFYEKA ATLETICO HUKO HUKO KWAO VICENTE CALDERON! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 20, 2016

EL DERBI MADRILEÑO: RONALDO HETITRIKI, REAL YAIFYEKA ATLETICO HUKO HUKO KWAO VICENTE CALDERON!


DABI ya Jiji la Madrid huko Spain, ambayo Jina la ubatizo ni ‘El Derbi Madrileño’, kati ya Atletico Madrid na Real Madrid ilichezwa Jana kwenye Uwanja wa Vicente Calderon na Vinara wa La Liga Real kuibuka kidedea kwa Bao 3-0 ambazo zote zilifungwa na Cristiano Ronaldo.

Hiyo ikiwa ni Dabi ya mwisho kuchezewa Uwanjani Vicente Calderon kwani Msimu ujao Atletico wanahamia Uwanja mpya na Ronaldo ndie alikuwa mwiba akipiga Hetitriki yake ya 39 katika Maisha yake ya Soka.

Ronaldo alifunga Bao la Kwanza Dakika ya 23 kwa Frikiki na Bao la Pili Dakika ya 71 kwa Penati na kumaliza la mwisho Dakika ya 77.


JE WAJUA?
Uso kwa Uso:
-Real Wameshinda Mechi 109
-Sare 51
Atletico Wameshinda Mechi 54


Ushindi huo umewaweka Real Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili FC Barcelona ambao mapema Jana walitoka 0-0 na Malaga na pia kuwabwaga Atletico kuwa Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Real.

VIKOSI:
Atlético Madrid: Oblak, Juanfran, Savic, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Niguez, Carrasco, Torres, Griezmann
Akiba: Correa, Hernandez, Tiago, Gameiro, Gaitan, Moya, Vrsaljko.

Real Madrid: Navas, Carvajal, Varane, Nacho, Marcelo, Kovacic, Modric, Isco, Vazquez, Bale, Ronaldo
Akiba: Casilla, Danilo, Ramos, Coentrao, Asensio, Rodriguez, Benzema.
REFA: David Fernandez Borbalan

LA LIGA
Ratiba/Matokeo:
**Saa za Bongo
Ijumaa Novemba 18
Real Betis 2 Las Palmas 0
Jumamosi Novemba 19
Deportivo La Coruna 2 Sevilla FC 3
FC Barcelona 0 Malaga CF 0
SD Eibar 1 Celta de Vigo 0
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 3
Jumapili Novemba 20
1400 Deportivo Alaves v RCD Espanyol
1815 Valencia C.F v Granada CF
2030 Sporting Gijon v Real Sociedad
2245 Athletic de Bilbao v Villarreal CF
Jumatatu Novemba 21
2245 CD Leganes v Osasuna

No comments:

Post a Comment