DER KLASSIKER: AUBAMEYANG AIBEBA DORTMUND KUIBAMIZA BAYERN, ILA LEIPZIG WAKO JUU KILELENI! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 20, 2016

DER KLASSIKER: AUBAMEYANG AIBEBA DORTMUND KUIBAMIZA BAYERN, ILA LEIPZIG WAKO JUU KILELENI!



BUNDESLIGA


Matokeo:
Jumamosi Novemba 19
Borussia Dortmund 1 Bayern Munich 0
FSV Mainz 4 Sport-Club Freiburg 2
Borussia Monchengladbachv 1 FC Köln 2
FC Augsburg 0 Hertha BSC 0
SV Darmstadt 0 FC Ingolstadt 1
VfL Wolfsburg 0 FC Schalke 1

Borussia Dortmund wamewatungua Wapinzani wao wakubwa na Mabingwa Watetezi Bayern Munich 1-0 Jana kwenye Mechi ya Bundesliga, iitwayo "Der Klassiker", iliyochezwa huko Sugnal Iduna Park ikishuhudiwa na Watazamaji 81,000 na kuiacha Timu iliyopanda Daraja Leipzig kushika usukukani.

Bao la ushindi la Dortmund lilifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang katika Dakika ya 11 na kuifanya Dortmund ikamate Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 21 points, zikiwa ni Pointi 3 nyuma ya Bayern ambayo Jana ni kipigo chao cha kwanza cha Msimu.

RB Leipzig wako kileleni mwa Bundesliga, wakiwa hawajafungwa na Pointi 3 mbele ya Mabingwa Bayern, baada Ijumaa kuichapa Bayer Leverkusen 3-2.

No comments:

Post a Comment